BODI ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imesema udahili wa
wanafunzi wanaofanya mitihani ya bodi hiyo umepungua kutokana na woga wa
wanafunzi na somo la hesabu kuwa tatizo kubwa kwao.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Kaimu
Mkurugenzi wa Bodi hiyo, Godfrey Mbanyi alisema lengo la bodi hiyo ni
kudahili wanafunzi waliochukua kozi ya ununuzi na ugavi 2,000, Hata
hivyo, alisema tangu mwaka 2016, udahili umekuwa ukishuka ambapo katika
mtihani uliofanyika mwaka 2016, walifanya udahili kwa wanafunzi 1,519,
waliofanya mtihani ni 1,442, waliofaulu ni wanafunzi 660 na kati yao 745
wanarudia mitihani wakati wanafunzi 37 sawa na asilimia 2.6 walifeli.

No comments:
Post a Comment