Trump.Azishushia Matusi Nchi Za Afrika - VAN NEWS

Latest

Thursday, 11 January 2018

Trump.Azishushia Matusi Nchi Za Afrika

Mapema jana jioni Januari 11, 2018, Rais wa Marekani amewashutumu wahamiaji wanaoingia nchini humo kwa kuwatusi katika ofisi yake ndani ya Ikulu ya Whitehouse.

”Kwa nini tunawaruhusu watu hawa kutoka mataifa ‘machafu”? amesema Trump.

Rais Trump aliyasema hayo wakti akizungumza na wabunge wa Bunge la Seneti, taarifa hii ni kwa mujibu wa gazeti la The Washington Post.

Tamko hilo lilidaiwa kuwalenga watu kutoka Afrika, Haiti na El Salvador.

Ikulu ya Whitehouse haikukana tamko hilo ambalo lilithibitishwa na vyombo vyingine vya habari.

”Wanasiasa fulani wa Washington hupendelea kupigania mataifa ya kigeni, lakini Rais Trump atawapigania raia wa Marekani pekee” alisema pia msemaji wa White House.

Matamshi hayo ya Rais Trump yanajiri huku wabunge kutoka vyama vyote wakimtembelea kupendekeza mpango wa wahamaiji usiopendelea upande wowote.

Seneta wa Democratic,  Richard Durbin alikuwa akizungumza kuhusu vibali vya muda wa kuishi vinavyotolewa kwa raia wanaotoka katika mataifa yaliokumbwa na majanga, vita ama milipuko ya magonjwa, vilisema vyombo vya habari.

Kulingana gazeti la Washington Post, bwana Trump aliwaambia wabunge kwamba Marekani badala yake inachukua wahamiaji kutoka Norway, ambayo waziri wake mkuu alimtembelea Rais Trump siku ya Jumatano.

Seneta Lindsey Graham, ambaye ni mwanachama wa chama cha Republian kutoka Carolina Kusini pia alikuwa katika mkutano huo lakini hakuweza kuzungumzia kuhusu matusi hayo yaliotolewa na rais Trump.



No comments:

Post a Comment