Kocha Al Masry, Hossam Hassan ametangaza kikosi chake cha wachezaji 21 akiwemo mshambuliaji wa Burkina Faso, Aristide Bance tayari kwa mchezo dhidi ya Simba katika hatua ya 32 ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Miamba hiyo ya Port-Said wataivaa Simba Jumatano ijayo saa 12 jioni baada ya kuiondoa Green Buffaro ya Zambia.
Hossam atamkosa nyota wake Islam Serry, ambaye ameumia wakati wa mchezo wa Al Masry walioshinda 2-1 dhidi ya Arab Contractors katika Ligi Kuu Misri.
Hata hivyo, kocha huyo amewachukua nyota wake wote wakiwemo Abdallah El-Shamy, Aristide Bance, Saeed Mourad na Ahmed Gomaa.
Kikosi cha Al Masry
Makipa: Ahmed Masoud, Mahmoud El-Sayed, Ahmed Busca.
Mabeki: Islam Salah, Mohamed Shatta, Ahmed Abd El-Mawgod, Abdallah El-Shamy, Mohamed Hamdy, Mohamed Koffi.
No comments:
Post a Comment