Video hiyo inaonyesha chumba ambacho yanga walitakiwa kutumia kubadilishia lakina hawakukitumia
Wachezaji wa Yanga walilazimika kugomea kuingia katika vyumba vya kubadilishia nguo baada ya kubaini kumepulizwa dawa ya kuwapunguza nguvu.
Wachezaji wa Yanga waliingia uwanjani kwa miguu wakitumia geti kuu (geti la kuingilia viongozi) na basi lao likiingia likiwa tupu.
Wachezaji na benchi la ufundi hawakuingia kwenye cha chumba kubadilishia nguo, walikaa nje ya chumba hicho huku baadhi ya viongozi wa Yanga wakionekana kuingia na kutoka chumba hicho.
Meneja wa Yanga, Saleh Hafidh alisema chumba walichotakiwa kubadilishia nguo wachezaji wao kilipuliziwa dawa.
“Hatuwezi kuingia katika chumba hiki kilichopuliziwa dawa, kama vipi tupewe chumba cha Lipuli na wao waje kwetu,” alisema Hafidh.
Hata hivyo madai hayo yalipigwa na Meneja wa Uwanja wa Samora-Iringa, Lazaro Manila alisema madai ya chumba chao kupiliziwa dawa yenye harufu mbaya siyo kweli.
“Hawa wameingiwa hofu inayoambatana na imani potofu za kishirikina na wanachokitafuta ni kupigwa faini tu ya kugoma kuingia ndani,” alisema Manila.
Aidha kikosi cha Lipuli nacho kiliingia uwanjani kwa kutumia geti kuu la kuingilia viongozi na kuliacha basi lao kuingia uwanjani likiwa tupu.
No comments:
Post a Comment