Jose Mourinho ametoa ruhusa kwa Manchester United kumrejesha Cristiano Ronaldo Old Trafford kutoka Real Madrid. United huenda wakalazimika kulipa pauni milioni 352 kumsajili. (La Sexta)
Manchester City wanataka kumsajili kiungo kutoka Ujerumani Emre Can, 24, anayechezea Liverpool, lakini mustakbali wake utategemea kama Liverpool watafanikiwa kumsajili Leon Groetzka, 22, kutoka Schalke. (Mirror)
Leon Groetzka wa Schalke amesaini mkataba wa awali na Bayern Munich na atajiunga nao mwisho wa msimu huu. (Sky Sports)
Matumaini ya Barcelona ya kumsajili Antoine Griezmann yamesita kidogo baada ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa kupata simu kutoka Manchester City. (Don Balon)
Tottenham watapambana na Manchester United katika kutaka kumsajili mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Lucas Moura, 25. (L’Equipe)
Arsenal wana uhakika wa kumsajili Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Borussia Dortmund na Henrikh Mkhitayran kutoka Manchester United mwezi huu. Arsenal tayari wamekubaliana maslahi binafsi na wachezaji wote wawili. (Goal)
Arsenal wapo hatua moja tu katika kukamilisha usajili wa Pierre-Emerick Aubameyang, 28, baada ya mchezaji huyo kuachwa katika kikosi cha kwanza cha Borussia Dortmund kitakachocheza na Hertha Berlin. (Bild)
Olivier Giroud huenda akajiunga na Borussia Dortmund katika mkataba wa Pierre-Emerick Aubameyang kwenda Emirates. (Daily Mirror)
Arsene Wenger amekata tamaa ya kutoweza kumzuia Alexis Sanchez kuondoka na anaamini mashabiki wa Arsenal watamuelewa, huku akidai kuwa kuondoka kwa Robin van Persie kwenda Manchester United mwaka 2012 ndio kuliuma zaidi. (Goal)
Mesut Ozil na Jack Wilshere wanajiandaa kusaini mkataba mpya wa kubakia Emirates. (Sun)
Chelsea huenda wakakabiliwa na adhabu ya kutosajili baada ya kuvunja sheria za usajili kwa kuchukua vijana wa chini ya umri wa miaka 18 kutoka nje ya England. (Guardian)
Leicester City wapo tayari kupambana na timu nyingine katika kutaka kumsajili beki Jonny Evans kutoka West Brom. (Daily Mail)
Inter Milan na Roma zinafikiria kutaka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge. (Football Italia)
Brighton wanataka kumsajili mshambuliaji wa PSV Eindhoven Jurgen Locadia, 24. (De Telegraaf)
Chelsea wamemuulizia mshambuliaji wa Stoke City Peter Crouch, 36, kufuatia kuumia kwa Andy Carroll, 29, wa West Ham waliyekuwa wakimnyatia. (Telegraph)
Stoke City wamesema hawajapata taarifa zozote kuhusu Peter Crouch kwenda Chelsea. (Sky Sports News)
Chelsea wanataka kumsajili Edin Dzeko, 31, na beki wa kushoto Emerson Palmieri, 23, kutoka Roma kwa jumla ya pauni milioni 77. (Daily Star)
Chelsea huenda wakamtumia Mitchy Batshuayi , 24, kama chambo katika kutaka kumsajili Edin Dzeko. (Sky Italia)
Kipa wa Manchester United David de Gea, 27, amesema kuwa sehemu ya United ni “jambo la kipekee” huku akijaribu kuzima tetesi kuhusu hatma yake Old Trafford. (ESPN)
Manchester United wana matumaini kuwa Alexis Sanchez atacheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Burnley siku ya Jumamosi. (Manchester Evening News)

No comments:
Post a Comment