YA 1998 KUJIRUDIA 2018 JANGWANI? - VAN NEWS

Latest

Friday, 23 February 2018

YA 1998 KUJIRUDIA 2018 JANGWANI?

HISTORIA INAJIRUDIA

Mwaka 1998 Timu Ya YANGA SC Ilikumbwa Na Ukata Wa Fedha Baada Ya Aliyekua Mfadhili Wa Timu Kipindi Hicho Marehemu 
Abasy Gulamali Kuingia Mitini Huku Timu Ikiwa Haina Hata Tshs 100/=

Kitendo Hicho Kilisababisha Wachezaji Tegemez Wote Akiwamo Edibily Jonas Lunyamila Wagome Na Wakati Huo Timu Ilikua Katika Ligi Tatu; 
NYERERE CUP, VPL Na
 CLUB BINGWA AFRICA, Kutokana Na Hali Hiyo Aliyekua Kocha Wa Yanga Enzi Hizo Tito Mwaluvanda Ikabidi Awatumie Wachezaji Chipukizi Akiwemo

Azizi Hunter.

Kikosi Hicho Cha Wachezaji Chipukizi Kilipewa Jina La 
YANGA YOSSO

#Mafanikio Ya YANGA YOSSO Yalikua Kama Ifuatavyo;

- Waliweza Kutinga Robo Fainal Ya Ligi Ya Mabingwa Africa

- Waliweza Kutetea Taji La Vpl Kwa Mara Ya Tatu Mfululizo

- Waliweza Kutwaa Kombe La Nyerere Kwa Kuwafunga 2 - 0 Simba Sc Katika Uwanja Wa Sheikh Amri Abeid Pale Arusha

Je hii yaweza kujitokeza mwaka huu 
Hili ni swali ambalo kila mpenzi na shabiku wa yanga anajiuliza kutokana na mwenendo wa kusua sua wa klabu hiyo 
Mwenendo huo unatokana na ukata unao isumbua klabu hiyo huku ikishuhudiwa wachezaji wake wengi hasa wakigeni wakisumbuliwa na majeraha ya muda mrefu huku mitaani kukiwa na tetesi huenda nyota hao wana mgomo unaosababishwa na ukata klabuni hapo
Hali hiyo inamfanya kocho kuwatumia zaidi vijana wadogo katika  michezo yake ya vpl,FA na ile ya klabu bingwa ..
Je ni kweli histiria hiyo inaweza kujirudia tena kwaka huu.

Kwa makala nyingi za kimichezo usikise kutembelea blog yetu vannewstz

No comments:

Post a Comment